Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Somalia yaomba Marekani kuisaidia kuwazuia al-shabab kuchimba madini ya Uranium
Serikali ya Somalia imetuma ombi la msaada wa kijeshi kwa Marekani, kuwazuia wanamgambo wa al-Shabab kuchimba madini ya uranium ya kuyatuma hadi nchini Iran.
Kwenye barua waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Yusuf Garaad, alisema kuwa wanamgambo hao wameteka eneo lenye madini ya uranium na wamekuwa wakichimba madini hayo.
Somalia inatajwa kuwa yenye madini ya uranium kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la kimataifa la kudhibti nishati ya nyuklia
Madai hayo hayajathibitishwa rasmi kuhusu vile uchimbaji huo wa madini ufanywa au ni kwa njia ipi al-Shabab inatuma madini hayo kweda Iran.
Barua hiyo ilesema kuwa al-Shabab inahusiana na kundi lijulikanalo kama Islamic State wakati limefahamika kuwa na uhusiano wa muda mrefu na al-Qaeda.
Ilisema kuwa tatizo la sasa ni kubwa hata kukishinda kikosi cha Muunganoi wa Afrika kilicho nchini Somalia.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni haijajibu barua hiyo lakini vyombo vya habari vinasema kwa Marekani ilithibitisha kuipokea barua hiyo.