Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nkurunziza afika Tanzania ziara yake ya kwanza nje tangu 2015
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anafanya ziara yake ya kwanza ya kigeni tangu kufeli kwa jaribio la kupindua serikali yake zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Amesafiri na mawaziri kadha kwenda nchini Tanzania, ambao imetoa makao kwa zaidi ya wakimbizi robo milioni kutoka Burundi.
Watu hao waliikimbia Burundi baada ya mzozo uliotokana na hatua ya Bw Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Nkurunziza alikuwa akihudhuria mkutano nchini Tanzania wakati jaribo hilo lilipofanyika mwezi Mei mwaka 2015.
Mamia ya watu wameuawa tangu mzozo huo uanze wengi wanaodaiwa kuwa wafuasi wa upinzani.