Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Madonna kufungua hospitali ya watoto Malawi
Nyota wa muziki kutoka Marekani Madonna anatarajiwa kufungua tawi jipya la hospitali ya watoto katika mji wa pili kwa ukubwa wa Blantyre nchini Malawi iliotegnezwa kupitia hazina yake ya Raising Malawi .
Hospitali hiyo ya Mercy and James inatumia majina ya watoto wawili wa madonna kati ya wanne anaowalea kutoka Malawi.
Tawi hilo la Hospitali hiyo ya watoto limechukua takriban miaka miwili kujenga na lina vyumba vitatu vya kufanya upasuaji na wadi yenye vitanda hamsini.
Ni hospitali ya kwanza yenye wataalam wa watoto katika taifa hilo lililopo kusini mwa Afrika hivyobasi kuongeza idadi ya uangalizi wa watoto katika hospitali ya Queen Elizabeth, ripoti hiyo imesema.
Rais Peter Mutharika anatarajiwa kuhudhuria sherehe za ufunguzi wake ,kulingana na ripoti.
Madonna alituma kanda ya video ya tawi hilo jipya katika mtandao wa Twitter.
Madonna alianzisha shirika hilo la hisani nchini Malawi 2006 na amekuwa mgeni wa kila mara nchini humo.