Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ukrain: Urusi ilihusika na udukuzi wa mitandao
Ukrain inasema ina ushahidi kuwa idara za usalama nchini urusi zilihusika kwenye udukuzi wa mitandao ambao ulilenga biashara kote duniani mapema wiki hii.
Makampuni ya Ukrain yalikuwa miongoni mwa yale ya kwanza kuripoti udukuzi huo siku ya Jumanne.
Urusi ilikana kuhusika na kuongeza kuwa madai hayo ni ya uwongo.
Kirusi kilichovuruga huduma za mitandao kote duniani kilitaka kulipwa fidia.
Hata hivo udukuzi huo pia ulikumba makampuni ya Urusi na kusababisha wataalamu wa mitandao kuseme kuwa Urusi haukuhisika.
Idara ya usalama nchini Ukrain ilisema fidia iliyoombwa ilikuwa ni ya kufunika na kuongeza kwa udekuzi huo ulilenga kuvuruga nmakapuiaya kibinafsi na ya serikali nchini Ukrain kwa lengo la kuzua msukosuko wa kisiasa.