Mlanguzi maarufu wa mihadarati aliyebadlisha sura akamatwa Brazil

Chanzo cha picha, Policia Federal
Polisi nchini Brazil wamamkamata mlanguzi wa madawa ya kulevya maarufu ambaye amefanyiwa upasuaji kubadilisha sura yake ili kukwepa kukamatwa kwa muda wa karibu miaka 30.
Luiz Carlos da Rocha ambaye pia anafahamika kama "White Head" anaaminika kuongoza genge kubwa la madawa ya kulevya barani America Kusini.
Polisi walisema kuwa hakumu anayoweza kupewa Rocha inaweza kuwa ya karibu miaka 50 jela.
Rocha alikamatwa eneo la Sorriso katika jimo la magharibu la Mato Grosson siku ya Jumamosi.

Chanzo cha picha, EPA
Amekuwa akiishi mjni humo akitumia jina Vitor Luiz de Moraes.
Polisi walilinganisha picha za zamani za Rocha na za mshukiwa mpya na kusema kuwa Luiz Carlos da Rocha na Vitor Luiz ni mtu mmoja.
Polisi wa Brazil wanasema kuwa genge lake lilitambuliwa kama lenye ghasia ambalo lilikuwa likitumia maghari yasiyopenya risasi na silaha nzito.
Genge hilo lilizalisha madawa ya Cocaine nchinin Bolivia, Peru na Colombia kabla ya kusafirisha madawa hayo hadi barani Ulaya na Marekani.












