Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wakenya na Wasomali 72 watimuliwa Marekani
Serikali ya Marekani imewatimua watu 72 kutoka Kenya na Somalia kutokana na matatizo mbalimbali ya uhamiaji.
Waliofurushwa ni Wakenya watano na hao wengine wana asili ya Kisomali, gazeti la Star limeripoti.
Afisa mmoja wa serikali ameambia BBC kwamba ni kweli watu hao wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi lakini akasema serikali ya Kenya bado inatafuta taarifa zaidi kuhusu utambulisho wao na uraia.
Waliwasili uwanja wa ndege mapema Ijumaa.
Mwezi Januari, Wakenya wawili na Wasomali 90 waliwasili uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta baada ya kufukuzwa Marekani kutokana na matatizo mbalimbali ya uhamiaji.
Rais wa Marekani Donald Trump ameahidi kukabiliana na wahamiaji haramu walio nchini Marekani tangu aingie madarakani mwezi Januari.