Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waziri aliyeuawa azikwa Somalia
Waziri wa ujenzi nchini Somalia aliyeuawa na na mwanajeshi wa serikali mjini Mogadishu siku ya Jumatano Abbas Abdullahi Siraji amezikwa katika mazishi ya kitaifa.
Mmoja wa wanajeshi wa serikali alifyatua risasi katika gari la waziri huyo alipokua akikaribia ikulu ya Rais.
Maafisa wa usalama wanasema kuwa mlinzi huyo alidhani gari hilo lingeleta madhara kiusalama na hakujua kuwa lilikuwa la waziri huyo.
Rais Mohammed Abdullahi Farmajo ameamuru kufanyika kwa uchunguzi wa kina.
Ameahirisha pia safari yake ya kikazi nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria mazishi hayo.
Abbas alikua mkimbizi katika kambi ya Dadaab na baadae kuwa waziri mdogo zaidi nchini humo huku akihamasiaha raia wengi wa nchi hiyo.