Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Arsenal yaifuata Chelsea fainali ya FA kwa kulaza Manchester City
Washika mitutu wa London klabu ya Arsenal imetinga fainali ya kombe la kombe Fa baada ya kuwachapa Manchester City kwa mabao 2-1 .
Mchezo huo wa nusu fainali ulichukua dakika 120 baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 katika dakika tisini za muda wa kawaida.
Man City ndio walioanza kuzifumani nyavu za Arsenal kwa goli la dakika ya 62 liliowekwa kambani na mshambuliaji wake mahiri Sergio Aguero Kun.
Beki wa kushoto wa Arsenal Nacho Monreal alisawazisha bao lilo katika dakika ya 71 ya mchezo .
Alexis Sanchez aliipeleka timu yake fainali kwa goli alilofunga katika dakika ya 101, kwa kufuatia patashika ya mpira wa kutengwa iliyotokea kwenye goli la City.
Fainali ya mchezo wa kombe la FA utapigwa Mei 27 katika dimba la Wembley ambapo Arsena watakipiga na Chelsea kuwania ubingwa wa kikombe hicho.