Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa Picha: Jinsi wakimbizi Uganda wanavyopata maji
Mamia ya maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan kusini wamekimbia vita na njaa katika nchi yao na kutafuta usalama katika kambi zilizo kaskazini Uganda.
Zaidi ya wakimbizi 50,000 sasa wanaishi katika kambi ya Rhino ambayo imejaa vibanda na mahema karibu na mji wa Arua.
Maisha katika kambi hiyo ni ngumu, lakini wote wanakubaliana kuwa moja ya changamoto kali ni ukosefu wa maji.
Hamna mabwawa ya maji, na mito michache ambayo hupitia eneo hilo imekauka. Na kama haijakauka kabisa, maji yake ni kama matope.
Wakiongea kuhusu uhaba wa maji, shirika la msalaba mwekundu limeamua kusafirisha maji kutoka mto Nile, ambayo yanapimwa, yanatibiwa halafu yanapimwa tena kabla ya kuwekwa kwenye malori.
Baadaye yanaendeshwa yakipitia msituni hadi katika kambi, ambapo yanamiminwa ndani ya mamia ya matangi madogo, ambayo yanajazwa mara mbili au tatu kila siku.
Wakitumia mabomba na mashine kupandisha maji, maji huvutwa kutoka kwa mto hadi ndani ya matangi ambapo yanaongezewa kemikali ya aluminium sulphate ya kutoa masimbi.
Mradi huo ulioanza kutoa maji mapema mwezi huu, sasa umeajiri zaidi ya watu 40 kutoka nchini na mataifa ya kigeni.
Noor Pwani, mmoja wa wafanyikazi katika shirika la msalaba mwekundu alisema kuwa hiyo ndio njia pekee ambayo wangepambana na magonjwa ya kuambukiza, ambayo huleta wasiwasi mkubwa haswa ikizingatiwa hali duni ya mazingira katika kambi zilizojaa huku mvua ikitarajiwa kunyesha hivi karibuni ambapo huwa chanzo cha magonjwa yanayosababishwa na maji.
Agaba Derrick ambaye anafanya kazi ya kujitolea huwa na jukumu la kuangalia jinsi maji ya mto yalivyo.
Matokeo ya utafiti wake huamua kiwango cha aluminium sulphate kitakachoongezwa. Klorini pia huongezwa ili kuua bakteria waliobaki.
Wakati maji yanapotiririka upande mwingine, huonekana kuwa ni safi. Mradi huo unatayarishwa kutoa mamilioni ya lita ya maji kila siku.
Kiwango kinachotumiwa na mtu mmoja kila siku katika kambi ni kati la lita 15-20 ambayo hutumika kufua, kupika na kunywa.
Msafara wa malori takriban 30 husafirisha maji safi hadi maeneo ya usambazaji katika kambi, ambayo hujazwa mara tatu kila siku.
Katika maeneo mengine barabara ililazimika kukarabatiwa ili kuweza kustahimili malori kupitia hapo.
Monica Achan, ambaye alitembea msituni kwa wiki mbili hadi Uganda baada ya shemeji yake kuuliwa na wanajeshi, anakunywa maji kutoka mto Nile katika makaazi yake mapya ndani ya kambi.
" Maisha ni magumu hapa, alisema. " Lakini tukiwa na maji tutaishi kwani maji ni uhai"
Picha na Ripoti na Tommy Trenchard.