Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vyama vya siasa vyaruhusiwa kujihesabia kura Kenya
Tume ya uchaguzi nchini Kenya imekubali kuruhusu vyama vya kisiasa kujihesabia kura kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.
Hata hivyo tume hiyo ilisema kuwa ndiyo ina ruhusa ya kutangaza matokeo ya mwisho.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alizua wasi wasi mwishoni mwa wiki baada ya kuwaambia wafuasi wake kuwa muungano wa upinzani wa Nasa, utabuni kituo chake cha kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Viongozi wa upinzani wanasema kuwa kuwepo kituo hicho itasaidia kuzuia udanganyifu kwenye uchaguzi.
Rais Uhuru Kenyatta anawania uchaguzi kwenye muhula wa pili na anatarajia kuukabili mungano wa vyama vikuu vya upinzani.