Ukame: Mifugo wengi waangamia Puntland

Athari za ukame mbaya eneo linalojitawala nchini Somalia la Puntland, zinazidi kuwa mbaya huku wafugaji wakiwapoteza mifugo wengi.

Licha ya kutembea safari ndefu kutafuta malisho na maji, wafugaji hawajafanikiwa kuwakoa mifugo wao kutokana na ukame huo.

Mashirika ya kibinanadamu yakiwemo ya chakula ya Umoja wa Mataifa, yamekuwa yakitoa maji na misaada mingine majuma machache yaliyopita.

Mifugo wamekuw wakidhoofika baada ya kushinda kwa siku kadha bila maji na chakula.

Waliobahatika walisafiriwa kwa magari kwa siku kadha.

Wafugaji hao wameacha familia zao na kusafiri mbali kutafuta malisho.

Familia moja inasema kuwa imepoteza mifugo 800 wakiwemo mbuzi na kondoo kwa kipindi cha mwezi mmoja.