Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Harusi 'ya Game of Thrones' yafanyika Marekani
Mashabiki sugu wa mwendelezo wa filamu za Game of Thrones waliamua kupiga hatua zaidi katika ushabiki wao kwa kufanya harusi ambayo iliiga filamu hiyo.
Makala mpya ya filamu hizo itatolewa katika kipindi cha miezi saba ijayo.
Mpiga picha Katie Lee anasema aliamua kuchukua hatua hiyo kujikumbusha kuhusu filamu hizo azipendazo sana.
"Nilijua kwamba lingekuwa jambo ngumu kufanikisha, nikiwa bado nahakikisha kwamba inakuwa harusi ya kufana," aliambia BBC.
Kulikuwa hata na mbweha - mbwa aliyepambwa kufanana na mbweha - kukamilisha muonekano wa Game of Thrones.
Katie alihamasishwa zaidi na wahusika awapendao zaidi Daenerys Targaryen na Sansa Stark.
Erin Foley aliyehusika katika mitindo na mavazi katika harusi hiyo anasema ndiyo yake aliyoifurahia zaidi na kwamba anajivunia pongezi ambazo amekuwa akipokea.
Bila shaka, Game of Thrones haiwezi kukamilika bila mbweha.
"Nilitaka sana kuongeza mbweha," anasema Katie.
"Nilijua ingeboresha picha za harusi zaidi."
Walimtafuta mbwa kwa jina River katika kituo cha kutunza mbwa walioteswa na wamiliki wao na kutelekezwa.
Harusi hiyo ilifanyika katika jumba la Smithmore ambalo linapatikana katika shamba la eka 121 katika mlima wa Blue Ridge, mashariki mwa Marekani.
Keki ilikuwa na sifa za zimwi, kwa heshima ya Daenerys, Mama wa Mazimwi.