Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uber yaondoa magari yanayojiendesha barabarani baada ya ajali
Kampuni ya Uber imeondoa magari yake yanayojiendesha barabarani, baada ya ajali ambapo moja ya magari yake lilianguka.
Picha zilizochapishwa zilionyesha gari lilokuwa limepinduka kwenye barabara katika jimbo la Arizona, kando na gari lingine lililokuw limeharibika vibaya.
Gari hilo aina ya Volvo SUV lilikuwa likijiendesha lenyewe wakati wa ajali. Hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Msemaji wa polisi eneo la Tembe huko Arizona, alisema kuwa ajalia hiyo ilitokea wakati gari lingine la Uber lilishindwa kugeuka upande wa kushoto.
Magari ya Uber yanayojiendesha kala mara huwa na mtu kwenye kiti cha dereva ambaye anaweza kuchukua usukani.
Kisa hicho kinajiri majuma kadha baada ya kampuni hiyo ya texi, kukumbwa na taarifa zisizo za kuridhisha zinazohusu mazingira ya kufanya kazi.