Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Aliyejaribu kumpokonya bunduki mlinzi auawa Ufaransa
Wizara ya mambo ya ndani nchini Ufaransa inasema mwanamume amepigwa risasi na kuuawa, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Orly, karibu na Paris, baada ya mwanamume huyo kunyakua bunduki ya mwanajeshi aliyekuwa katika zamu ya ulinzi.
Hakuna mtu mwengine aliyejeruhiwa.
Wataalamu wa kutegua mabomu, waliofanya ukaguzi, wanasema mwanamume huyo hajakutikana na mabomu yoyote.
Watu wamehamishwa kutoka uwanja huo wa ndege, na ndege zimeelekezwa kutua katika uwanja mwengine wa Charles De Gaulle.
Katika tukio jengine, afisa wa polisi alipigwa risasi na kujeruhiwa, wakati wa ukaguzi wa kawaida katika barabara kaskazini mwa Paris.
Haijulikani kama matukio hayo mawili yanahusiana.
Wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa inasema polisi wamekuwa wakimjua mwanamume huyo, na wamekuwa wakimchunguza.