China yalipiza hatua ya kuwekwa makombora Korea Kusini

Chanzo cha picha, Reuters
China ni soko muhimu kwa makampuni mengi ya Korea Kusini, lakini hata kampuni ya maduka ya jumla ya Lotte haijatengwa,
Kampuni hiyo nambari tano kwa ukubwa nchini Korea Kusini, inapata takriban asilimia 30 ya mauzo yake kutoka China na huwaajiri watu 20,000 nchini humo.
Lakini kwa kipindi cha wiki moja iliyopita, biashara zake zimekumbwa na upinzani kutoka kwa wadukuzi, wateja na washirika.
Siku ya Jumatutu Lotte ilisema kuwa zaidi ya maduka yake 10 kote nchini humo yalifungwa kwa ghafla
Hadi mwishoni mwa mwezi Februari Lotte ilikubali kutoa ardhi iliyokuwa ikimiliki nchini Korea Kusini pamoja na uwanja wa gofu, ili Marekani iweze kujenga mitambo yenye utata ya makombora ya kujikinga yanayofahamika kama THAAD.
Yakiwa na uwezo wa kudungua makombora, Marekani inasema kuwa ni kingi muhimu dhidii ya Korea Kaskazini.
Lakini kwa miaka michache iliyopita China imekuwa ikipinga hatua hiyo ikisema kuwa mitambo hiyo ina uwezo wa kuipeleleza China.
Inapinga madai kuwa mitambo hjiyo itasaidia kuleta udhabiti ikisema kuwa hastahili kuruhusiwa kuendelea.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, EPA












