Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wakili: Mwana wa Muhammad Ali alizuiliwa kuingia Marekani
Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kwamba mwana wa aliyekuwa gwiji wa ndondi nchini Marekani Muhammad Ali alizuiliwa na kuhojiwa kwa saa mbili katika uwanja wa ndege wa Florida baada ya kuwasili kutoka Jamaica mapema mwezi huu kutokana na jina lake la Kiarabu.
Wakili wa familia ya Muhammd Ali Chris Mancini alinukuliwa akisema kuwa kuzuiliwa kwa Muhammad Ali Jnr kulihusishwa moja kwa moja na jaribio la rais Trump kuwapiga marufuku Waislamu kutoka mataifa saba ya Waislamu kuingia Marekani.
Kwengineko mcheza filamu mmoja kutoka Syria ambaye alishiriki katika filamu ilioteuliwa kuwania tuzo za Oscar amezuiliwa kuelekea katika sherehe za tuzo hizo mjini Los Angeles
Kulingana chombo cha habari cha AP, Khaleed Khateeb alipewa Visa ya Marekani lakini akazuiliwa kupanda ndege iliokuwa ikielekea Marekani .
Kampuni hiyo ya ndege imesema kuwa maafisa wamepata habari mbaya kumuhusu