Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanafunzi wauawa kwa kupigwa risasi Guinea
Takriban watu watano wameuawa nchini Guinea wakati vikosi vya usalama vilipopambana na wanafunzi waliokuwa wakiandana wakitaka mgomo wa walimu kumalizika.
Wanafunzi walijitokeza kwa wingi na kwa hasira wakaanza kuwatupia polisi mawe.
Maafisa walithibitisha vifo hivyo na kuwalaumu waandalizi wa maandamano kwa kupanga kile kilichotajwa kuwa maandamano haramu.
Mfanyakazi mmoja wa hospitali aliliambia shirika la AFP kuwa waliouawa walipigwa risasi kwa karibu na polisi wa kuzima maandamano.
Takriban watu 30 walijeruhiwa wakiwemo maafisa wa vikosi vya usalama.
Waalimu nchini Guina wamekuwa kwenye mgomo wakilalamikia mishahara duni.