Pacha waliotenganishwa Kenya watembezwa nje ya hospitali

Blessing na Favour wakiwa na mama yao

Chanzo cha picha, Kenyatta National Hospital

Pacha waliozaliwa wakiwa wameshikana sehemu ya chini ya mgongo lakini wakatenganishwa na madaktari hospitali kuu ya taifa ya Kenyatta, Nairobi Novemba mwaka jana, walifanya matembezi yao ya kwanza jana nje ya hospitali hiyo.

Watoto hao Blessing na Favor walitembezwa katika kituo cha wanyamapori cha Animal Orphanage, Nairobi kuwaona wanyama Siku ya Wapendanao.

Ilikuwa mara yao ya kwanza kutoka hospitalini tangu walipolazwa 5 Septemba, 2014.

Pacha hao walifanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha, ambao ulitajwa na wengi kuwa ufanisi mkubwa wa madaktari Kenyatta, tarehe 2 Novemba mwaka jana.

Afisa mkuu mtendaji wa hospitali hiyo Lily Koros Tare alisema acha hao wamepiga hatua sana tangu wafanyiwe upasuaji.

Blessing na Favour

Chanzo cha picha, Kenyatta National Hospital

Maelezo ya picha, Wakiondoka hospitalini
Blessing na Favour

Chanzo cha picha, Kenyatta National Hospital

Maelezo ya picha, Wakijionea simba
Blessing na Favour

Chanzo cha picha, Kenyatta National Hospital

Pacha waliotenganishwa

Chanzo cha picha, Kenyatta National Hospital