Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nyangumi wengine 240 wakwama ufukweni New Zealand
Wana mazingira nchini New Zealand, wanasema nyangumi wengine mia mbili na 40 wa aina ya "pilot", wamekwama katika ghuba ilioko mbali, kwenye kisiwa cha kusini cha New Zealand.
Kundi hilo jengine la nyangumi lilikwama kwenye ufukwe unaoitwa Farewell Spit, punde baada kundi la nyangumi mia moja kusaidiwa kurudi baharini maji yalipojaa.
Nyangumi mia tatu walikufa jana.
Eneo hilo la pwani la kilomita 20, lenye maji ya kina kifupi, ni gumu kwa nyangumi kuogelea.
Indaiwa kuwa huenda nyangmi hao walisukumwa hadi ufukweni na papa baada ya alama za kung'atwa kupatikana katika mmojawapo wa nyangumi hao aliokufa.
Hathivyo haijulikani ni kwa nini nyangumi hao wanaendelea kuwasili katika ufuo huo wa kilomita 5 karibu na Golden Bay.
Wataalam wanasema kuwa nyangumi ambao hujipata ufukweni hutoa wito kwa wenzao ambao nao pia hujipata katika ufukwe.