Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mhubiri awapa waumini dawa ya kuua panya Afrika Kusini
Mhubiri mmoja nchini Afrika Kusini amekuwa akiwapa waumia sumu ya kuua panya kama moja ya njia ya kujaribu imani yao.
Light Monyeki, ambaye anaongoza kanisa la Grace Living Hope Ministries mjini Pretorria, anasema kuwa kwa kunywa sumu hiyo, inaonyesha kuwa kifo hakina nguvu kwa waumini.
Picha kwenye ukurasa wake wa Facebook, zinamuonyesha akichanganya dawa inayotumiwa kuua panya wa chupa na kuinywa na kisha kuwapa waumini.
Bwana Monyeki ni mhubiri wa hivi majuzi kuripotiwa kuhusika na visa vyenye utata kanisani.