Ndege zatakiwa kubeba abiria wa nchi 7 za Waislamu kueleka Marekani

Kampuni ya ndege ya Qatar Airline
Maelezo ya picha, Kampuni ya ndege ya Qatar Airline

Idara ya forodha ya Marekani imeyaambia mashirika ya ndege kwamba waruhusu abiria kupanda ndege kuelekea Marekani abiria ambao walinyimwa ruhusa baada ya Rais Trump kutoa amri kwamba watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, wakataliwe kuingia Marekani.

Shirika la ndege la Ghuba, Qatar Airways, lilisema litaanza kupakia abiria haraka.

Hatua hiyo inafuata saa tu baada ya jaji wa mahakama ya taifa ya Marekani, kuzuia amri hiyo ya Rais Trump kwa muda.

Mahakama iliamua kuwa hatua ya rais ilivunja katiba, ambayo inakataza dini moja kupendelewa kushinda nyengine.

Mwanafunzi kutoka Iran aliyefurahishwa na hatu hiyo ya mahakama

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanafunzi kutoka Iran aliyefurahishwa na hatu hiyo ya mahakama

Serikali inasema itakata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Katika hotuba yake ya kila juma, rais alisema amri yake ilikusudiwa kuwalinda Wamarekani