Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Upepo wang'oa paa la jengo la bunge Ghana
Shughuli za ukarabati zinaendelea kwenye jengo ya bunge nchini ghana baada ya upepo mkali kung'oa sehemu zya paa la jengo hilo siku ya Jumanne jioni.
Kisa hicho kilisababisha kusitishwa vikao kwa ghafla wakati mvua ilianza kunyesha ndani ya jengo.
Wafanyakazi walijaribu kukinga baadhi ya maeneo yaliyoachwa wazi kwa kukusanya maji wakitumia ndoo.
Jengo hilo lililo kwenye mji mkuu Accra lilikarabatiwa miaka miwili iliyopita.