Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watoto milioni 18.6 walizaliwa China mwaka 2016
Idadi ya watoto wanaozaliwa nchini China ilikuwa ya juu zaidi tangu mwaka 2000 licha ya kushuka kwa idadi ya wanawake waliofikisha umri wa kuzaa, kwa mujibu wa maafisa nchini humo.
Kuongezeka huku kumetokana na china kuondoa sheria zake za mtoto mmoja mwaka mmoja uliopita.
Watoto milioni 18.6 walizaliwa mwaka 2016 ambalo ni ongezekeo la asilimia 11.5 kutoka mwaka 2015.
Zaidi ya asilimia 45 ya watoto waliozaliwa mwaka 2016 walikuwa na ndugu mmoja au wawili wakubwa.
Maafisa wanasema kuwa ifikapo mwaka 2020 kati ya watoto milioni 17 na 20 wanatarajiwa kuzaliwa nchini China kila mwaka.
Wanakadiria kuwa ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na zaidi ya watu milioni 30 zaidi watakaofanya kazi nchini China.
Sheria za kuzaa mtoto mmoja nchini China zilianza kutumika mwaka 1979 na zinaripotiwa kuchangia China kupoteza watu milioni 5 kila mwaka hali ambayo itashuhudiwa miaka kadha inayokuja