Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi za Uturuki wafanya mashambulizi ya pamoja Syria
Urusi na Uturuki zimefanya mashambulizi yao ya kwanza ya pamoja, dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria, kwa mujibu wa wizara ya ulinzi nchini Syria.
Islamic State ililengwa katika vitongoji vya mji wa al-Bab mkoani Aleppo, ambapo Uturuki ilikumbwa na maafa makubwa mwezi uliopita ikipigana na Islamic State.
Msemaji wa Urusi Luteni Sergei Rudskoi amesema kuwa mashambulizi hayo ya pamoja yamekuwa yenye mafanikio makubwa.
Urusi na Uturuki wamengilia pakubwa vita vya Syria.
Mji wa al-Bab ulio umbali wa kilomita 20 kutoka mpaka wa Uturuki, umekuwa ukilengwa na harakati za Uturuki zenye lengo la kuwatimua wanamgambo wa Islamic State na vikosi vya Kurdi.
Ndege za Marekani nazo ziliendesha mashambulizi mapema wiki hii pia kwa ushirikiano na Uturuki.