Popo nondo apewa jina la Donald Trump

Popo nondo mpya aliyegunduliwa mjini California nchini Marekani amepewa jina baada ya rais mteule wa Marekani Donald Trump.

Jina Neopalpa donaldtrumpi linatokana na nywele zinazofinika kichwa chake ambazo mtafiti huyo wa Canada anazifananisha na na reis huyo mteule.

Popo nondo huyo ambaye ni mdogo anatoka kusini mwa California na jimbo la Baja California nchini Mexico.

Ni aina ya kwanza ya popo kupewa jina la Trump.

Rais Obama ana aina tisa ya popo nondo walio na jina lake.