Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Netanyahu amuombea msamaha mwanajeshi aliyeua Israel
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anaunga mkono wito wa msamaha kwa mwanajeshi wa Israel aliyekutwa na hatia ya kuuwa bila kukusudia baada ya kumpiga risasi mshambuliaji wa Palestina aliyekutwa amelala chini akiwa na majeraha.
Waendesha mashtaka wamesema mauaji hayo yaliyotekelezwa na Elor Azaria Magharibi mwa benki iliyokuwa na watu wengi yalikuwa ni kitendo cha kulipiza kisasi.
Lakini viongozi mashuhuri katika Baraza la Mawaziri la bwana Netanyahu wamekosoa maamuzi hayo, ingiwa baba wa Raia huyo wa Palestina alisema maamuzi hayo yalikuwa yenye haki.
Mashtaka haya yameleta utengano mkubwa katika jamii ya Israel.
Jeshi limesema Sergeant Azaria amekiuka kanuni za maadili ya kijeshi lakini wanaomuunga mkono wanasema mwanajeshi huyo alikuwa anajilinda na kwamba viongozi wake wamemgeuka.