Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maandamano ya kumtaka Kabila kujiuzulu yafanyika duniani
Kumekuwa na maandamano katika miji kadhaa mikuu duniani ya kumtaka rais wa DR Congo Joseph Kabila kujiuzulu.
Leo ni siku ya mwisho ya utawala wake ,lakini uchaguzi umeahirishwa ambapo upinzani wa taifa hilo unasema kuwa ni jaribio la Kabila kusalia madarakani.
Katika mji mkuu wa Kinshasa na kwengineko, kuna idadi kubwa ya vikosi vya usalama na raia wameamua kusalia majumbani mwao.
Takriban watu 40 wamekamatwa katika mji wa mashariki wa Goma.
Mazungumzo na upinzani yanayofanywa na viongozi wa makanisa yamefeli kuafikia mwafaka, jaribio jingine la kuendeleza mazungumzo hayo litaendelea siku ya Jumatano.
Zaidi ya watu hamsini walifariki katika makabiliano ya barabarani mnamo mwezi Septemba.