Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jackie Evancho: Msichana atakayeimba sherehe ya kuapishwa kwa Trump
Jackie Evancho, aliyemaliza wa pili katika shindano la kutafuta watu wenye vipaji la America's Got Talent ndiye atakayeongoza wimbo wa taifa wakati wa kuapishwa kwa Donald Trump.
Msichana huyo wa miaka 16 amesema ana furaha sana kwamba atakuwa anaongoza wimbo huo wa taifa wakati wa sherehe hiyo tarehe 20 Januari.
Alimaliza wa pili katika shindano hilo mwaka 2010.
Boris Epshteyn, mkurugenzi wa mawasiliano wa kamati inayofanya maandalizi ya sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Bw Trump, amesema msichana huyo anawapa moyo Wamarekani wote.
Mwitaliano Andrea Bocelli na rapa Kanye West, ni miongoni mwa wasanii wengine ambao inadaiwa huenda wakatumbuiza siku hiyo.
Kanye West alikutana na rais huyo mteule katika jumba la Trump Tower jijini New York Jumanne.
Hata hivyo, hakujatolewa thibitisho kuhusu iwapo wawili hao walijadiliana kuhusu sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Trump.