Marekani kusimamisha uuzaji wa silaha kwa Saudi Arabia

Marekani imesema kuwa itasimamisha uuzaji wa silaha kwa nchi ya Saudi Arabia kwa sababu ya tuhuma kuwa ndege za Saudia zilihusika katika mashambulizi ya anga nchini Yemen.

Ofisa wa ngazi ya juu kutoka Washington amesema vikosi vya usalama vya Marekani vina ushahidi wote juu ya mashambulizi hayo.

Watetezi wa haki za binaadam wanasema kuwa mashambulizi hayo ya angani yaliharibu hospitali, shule na masoko huku wakitaja kama uhalifu wa kivita.

Serikali ya Saudi Arabia imekana tuhuma hizo na kusema haijawahi kulenga raia katika shambulizi lake lolote.