Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kampeni ya kupiga marufuku magari ya Diesel yaanza London
Kampeni mpya inayoongozwa na wafanyikazi wa huduma ya afya imeanzishwa mjini London kwa lengo la kupiga marufuku magari yote yanayotumia mafuta ya Diesel.
Madaktari dhidi ya Diesel wanasema kwamba takriban watu 9,400 mjini London hufariki kila mwaka kutokana na kupumua hewa chafu inayotoka katika magari yanayotumia Diesel.
Tayari miji ya Paris, Madrid, Mexico na Athens imethibitisha kwamba itapiga marufuku magari yote yanayotumia mafuta hayo.
Madaktari hao sasa wamemtaka Meya wa jiji la London Sadique Khan kuanza mpango wa kuyaondoa magari yanayotumia mafuta ya Diesel.
Tayari Bw Khan amenukuliwa akisema kuwa ana mpango wa kuyapiga marufuku mabasi yote yanayotumia mafuta hayo ifikiapo 2018.