Msanii maarufu zaidi katika Instagram 2016

Nyota wa muziki wa pop Selena Gomez ndiye msanii maarufu zaidi katika mtandao wa Instagram mwaka huu.

Ndiye mtu aliye na wafuasi wengi zaidi na pia ana picha nane kati ya 10 zilizopendwa zaidi na watumiaji wa mtandao huo mwaka huu, sawa na video saba kati ya 10 za wasanii zilizopendwa zaidi.

Instagram, kwenye takwimu zake za mwaka huu, wanasema wasanii wa kike ndio waliofanikiwa zaidi katika mtandao huo.

Selena Gomez ana wafuasi 103 milioni, ambazo anawazidi watu wengine wote ila akaunti ya Instagram yenyewe.

Nyota mwenzake wa Pop Taylor Swift, 24, ana wafuasi 94 milioni.

Swift alikuwa mtu mashuhuri zaidi katika Instagram mwaka 2015.

Baada ya wawili hao, kuna, Ariana Grande na Beyonce, kisha mwigizaji wa kipindi cha uhalisia runingani Kim Kardashian.

Kuanzia hapo ndipo anapotokea mwanamume wa kwanza, katika nafasi ya sita, nyota wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Picha ya Selena Gomez iliyopendwa zaidi ni moja ambapo anavumisha Coca-Cola.

Siku ambayo watu walitumia Instagram zaidi mwaka 2016 ni siku ya Halloween na kibonzo cha hisia (emoji) kilichotumiwa zaidi ni cha moyo.

Kendall Jenner ndiye aliyekuwa na picha maarufu zaidi mwaka 2015.