Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kanye West aondoka hospitalini
Mwanamuziki Kanye West anaripotiwa kurejea nyumbani zaidi ya wiki moja baada ya kulazwa kutokana na uchovu.
Kulingana na taarifa tofauti nchini Marekani, mwanamuzi huyo aliondoka hospitali ya UCLA jimbo la Los Angels na mkewe Kim Kardashian pamoja na daktari wake Michael Farzam,
Kanye West mwenye umri wa miaka 39 alilazwa hospitalini siku ya Jumatatu bada ya kupatwa na uchovu uliotokana na kukosa usingizi na kuishiwa na maji mwilini, kwa mjibu wa TMZ.
Nalo jarida la People limenukuu taarifa zinazo sema kuwa Kanye yuko nyumbani akiwa anapumzika.
Alitumia karibu muda wa dakika kumi akizungumza kuhusu Beyonce, Jay Z, Hillary Clinton na mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerbrg wakati kifanya shoo.
Mwanamitindo Kendal Jenner, ambaye ni dada wa kambo wa Kim Kardashian, alisema kuwa familia imekuwa ikimuombea Kanye.