Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump: Hesabu mpya ya kura Wisconsin ni kashfa
Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, ametaja mipango ya kuhesabu kura upya katika jimbo la Wisconsin kama kashfa.
Alisema kuwa hata mpinzani wake mkuu Hillary Clinton amekubali matokeo ya uchaguzi.
Bwana Trump alimshinda Bi Clinton kwa kura chache sana katika Wisconson lakini chama cha Green Party kimeomba rasmi kura hizo zihesabiwe tena ili kuhakikisha kuwa hakuna magendo yoyote yaliyofanywa.
Bwana Trump alisema kuwa kiongozi wa Green Party, Jill Stein, anajaribu kurejesha pesa alizopoteza wakati wa kampeni kwa kisingizio kuwa anataka kura kuhesabiwa upya.
Chama hicho pia kinakusudia kuchochea shughuli za kuhesabu kura upya katika majimbo ya Pennsylivania na Michingan.
Msemaji wa Bi Clinton alisema kuwa shughuli za kuhesabu upya kura zikianza, kundi lake litashiriki.
Lakini wachunguzi wa kisiasa wanasema kupunguza kura katika majimbo yote matatu ni jambo ambalo si rahisi.