Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Papa Francis asogeza mbele kusamehewa kwa wanawake wanaotoa mimba
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesogeza mbele kwa muda usiojulikana suala la mapadre wa kikatoliki duniani kusamehe wanawake walitoa mimba.
Mwaka jana aliwaruhusu mapadre kufanya hivyo kwa kipindi ambacho kilitajwa kama mwaka wa huruma ya Mungu kilichoisha Jumapili iliyopita.
Hapo awali maaskofu peke yao ndio waliokuwa na uwezo wa kuwasamehe wanawake waliotoa mimba.
Baba mtakatafu amesisitiza kwamba mafundisho ya kikatoliki yanaonyesha kwamba utoaji mimba ni kosa kubwa, lakini kiongozi huyo ameeleza kwamba Mungu ni mwenye huruma na anaweza kusamehe dhambi zote ikiwa mkosaji atatubu.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani amesema anaelewa jinsi suala la utoaji wa mimba linavyoweza kuwa tatizo kimaadili kwa mwanamke.