Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Soyinka: Nitaondoka Marekani Trump akiapishwa
Mshindi wa Tuzo la Nobel na mwandishi raia wa Nigeria Wole Soyinka, anasema kuwa ataondoka Marekani siku ambayo Donald Trump ataapishwa kuwa rais.
Wiki iliyopita Soyinka aliahidi kuwa angeirarua green Card yake, ikiwa Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.
Green Card humpa mtu kibali ya kuishi rasmi nchini Marekani na hupewa umuhimu mkubwa na wahamiaji kutoka nchi za Afrika.
Soyinka alitoa matamshi hayo wakati akihutubia wanafunzi katika chuo cha Oxford nchini Uingereza.
Mwandishi huyo maarufu alionekana kuchukua msimamo mkali kupinga seza za uhamiaji za bwana Trump.
Soyinka alishinda tuzo la Nobel la fasihi mwaka 1986 na kuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo hilo.