Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Samaki anayejiponya uti wa mgongo
Watafiti nchini Marekani wamesema wamebaini aina fulani ya samaki anayeweza kuzalisha upya uti wake wa mgongo unapovunjika wanaweza kusaidia kubuni matibabu yatakayoweza kuwasaidia watu waliopooza kutembea tena.
Wanasayansi wamegundua kuwa samaki huyo ajulikanaye kama Zebra Fish anapovunjika uti wa mgongo, huzalisha sehemu nyingine ya uti wa mgongo na kuunganisha kama daraja sehemu zilizokatika kwa kutumia aina ya protini mwilini mwake.
Wanadamu wanayo aina hiyo ya protini inayoweza kuzalisha mifupa lakini haifanyi kazi sawa na ile ya samaki huyo.
Aina hiyo ya protini kwenye binadamu inafanana kwa asilimia 90 na aina hiyo kwenye samaki hao.