Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ufaransa: Tumekamilisha kuondoa wahamiaji Calais
Serikali ya ufaransa inasema kuwa wamekamilisha uhamishaji wa maelfu ya wahamiaji katika kambi za Calais, maarufu kama jungle.
Uvunjwaji wa kambi hizo ulianza siku ya jumatatu huku wahamiaji wakisafirishwa kwa mabasi katika kambi mbalimbali za wakimbizi nchini humo.
Picha za televisheni zimeonesha moshi mweusi ukitokea kwenye mahema na duka ambayo huenda yamechomwa moto na wanaharakati wenye hasira au wahamiaji.
Lakini mbali na serikali ya nchi hiyo kusema kuwa kambi hiyo sasa haina watu, Dorothy Sang kutoka shirika la kutetea haki za watoto la save the children ameiambia BBC kuwa bado kuna wasiwasi juu ya idadi kubwa ya watoto wasio na wazazi ambao wanadhaniwa kuwepo bado katika kambi hiyo.