Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mahakama ya ICC yaisihi Burundi kutojiondoa
Mipango ya Burundi kutaka kujiondoa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imetajwa na bodi inayosimamia kazi ya mahakama hiyo kuwa 'pigo' katika vita dhidi ya watu wasioheshimu sheria.
Wiki iliopita ,bunge la Burundi liliidhinisha mpango wa baraza la mawaziri kukata uhusiano na mahakama hiyo ya mjini Hague.
Mipango ya Burundi kutaka kujiondoa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imetajwa na bodi inayosimamia kazi ya mahakama hiyo kuwa 'pigo'nisha mpango wa baraza la mawaziri kukata uhusiano na mahakama hiyo ya mjini Hague.
Mwendesha mashtaka wa ICC amesema kuwa atachunguza kile kilichotokea Burundi wakati wa maandamano dhidi ya rais Pierre Nkurunziza.
Aliyekuwa waziri wa haki nchini Senegal Sidiki Kaba,ambaye anaongoza bodi hiyo ya ICC ,alitoa wito kwa Burundi kuzungumzia wasiwasi wake badala ya kujiondoa katika mahakama hiyo.
Mwaka uliopita,marais wa Umoja wa Afrika walipitisha pendekezo kutafuta njia ambayo bara la Afrika lingeweza kujiondoa katika mahakama hiyo kwa pamoja.
Kumekuwa na malalamishi kwamba mahakama hiyo inalenga maswala ya Afrika pekee.
Kesi zote zinazoangaziwa na mahakama hiyo zinatoka Afrika.