Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
UN yatishia kuichukulia hatua Korea Kaskazini
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu vikali hatua ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu siku ya Jumatatu.
Pyongyang ilirusha makombora matatu baharini mkutano wa viongozi wa mataifa 20 yenye ushawishi mkubwa duniani ulipokuwa ukiendelea nchini China.
Kwenye azimio lililopitishwa kwa kauli moja na wanachama 15 wa baraza hilo, ikiwemo China - mshirika mkuu wa Korea Kaskazini - baraza hilo lilitishia kuchukua "hatua nyingine kali" dhidi ya taifa hilo lisipositisha majaribio ya mabomu ya nyuklia na makombora.
Korea Kaskazini imezuiwa na UN kutekeleza majaribio hayo na imekuwa ikiwekewa vikwazo mara kwa mara.