Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
China yanasa walaji rushwa waliotorokea ng’ambo
China imesema imefanikiwa kuwakamata na kuwarejesha nchini humo theluthi moja ya washukiwa wakuu wa ufisadi waliokuwa wametorokea nchi za nje.
Serikali ilizindua mpango wa kuwasaka washukiwa hao waliokabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kiuchumi miaka miwili iliyopita.
China imekuwa ikitafuta usaidizi kutoka kwa jamii ya kimataifa kuwakamata washukiwa hao lakini serikali nyingi zimekuwa zikikataa kuisaidia kutokana na wasiwasi kuhusu kuheshimiwa kwa haki za kibinadamu.
Lakini serikali imesema viongozi wa mataifa 20 yenye ushawishi mkubwa kiuchumi duniani (G20), ambao wamekuwa wakikutana mjini Hangzhou, China wamekubali kuunda kituo cha utafiti cha kuzingatia baadhi ya maombi.
Ufisadi huwa tatizo kubwa sana China na Rais Xi Jinping aliahidi kukabiliana nao.
Chama tawala kilisema mwaka uliopita kwamba watu 300,000 waliadhibiwa baada ya kupatikana na hatia mwaka jana.