Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wachuuzi waandamana Eastleigh, Nairobi
Mamia ya wachuuzi waliokasirika wamefanya maandamano katika barabara za eneo la Eastleigh jijini Nairobi ili kupinga kuvunjwa kwa vibanda vyao.
Usiku kucha maafisa wa polisi waliharibu vibanda vilivyojaa kandokando ya barabara ambapo huweka bidhaa zao zote.
Operesheni hiyo ya polisi inafuatia malalamishi kutoka kwa wamiliki wa maduka ambao wanasema kuwa wamekuwa wakizuia watu kuingia katika maduka hayo.
Wamiliki wa maduka pia nao wamefunga maduka yao ikiwa ni mgomo wao wa siku tatu wa kutaka baraza la jiji la Nairobi kuwandoa wachuuzi hao.