Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chuo kikuu kilichouza watumwa Washington, Marekani chajutia
Chuo kikuu kimoja nchini Marekani, ambacho kiliuza watumwa wakati biashara ya utumwa, kimeeleza kujutia kitendo hicho.
Chuo kikuu cha Georgetown, kinachopatikana mjini Washington DC, kimesema kitawapendelea wajukuu wa watumwa waliouzwa na chuo hicho karne ya 19 wakati wa kuwateua wanafunzi wa kujiunga na chuo hicho.
Mwaka 1838, chuo kikuu hicho kiliuza watu 272 ili kuweza kulipa madeni yake.
Waliouzwa walikuwa wanaume, wanawake na watoto.
Tukio hilo lilinakiliwa vyema na kwa sasa watafiti na wachunguzi wamefanikiwa kuwapata baadhi ya jamaa za watumwa waliouzwa.
Miongoni mwa hatua nyingine ambacho chuo hicho kinachukua ni kubadili majina ya majengo yake na kuyapa majina ya watumwa hao.
Aidha, chuo hicho kitafadhili taasisi mpya ya utafiti kuhusu utumwa.