Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Facebook yawapatia wateja fursa ya kutoa tahadhari
Mtandao wa facebook umewapatia fursa wateja wake kutoa ishara ya tahadhari ya kiusalama iwapo watajipata katika hali hatari.
Kufikia sasa huduma hiyo ilikuwa inaweza kutolewa na wafanyikazi wa kampuni hiyo pekee.
Huduma hiyo ya usalama inawapatia watumiaji wa mtandao huo fursa ya kutoa ujumbe kwa marafiki ama familia zao kwamba wako salama kunapotokea janga la kibinaadamu mahala walipo.
Tetemeko la ardhi la hivi majuzi nchini Itali liliadhimisha mara 25 mwaka huu kwamba lilisababishwa.
Ujumbe huo wa usalama umewafikia watu bilioni moja mwaka 2016 pekee,kampuni hiyo imesema.
Katika kipindi cha miaka 2 iliopita kwa pamoja huduma hiyo ikutumika mara 11 pekee.
Timu ya facebook inayotoa huduma hiyo hutumia vigezo vitatu kubaini kuamua iwapo huduma hiyo inapaswa kutolewa:
- Idadi ya watu walioathirika
- Athari ya janga hilo
- Na wakati wa tukio