John Kerry akwama kwenye foleni Delhi, India

Wageni mashuhuri wanapozuru mji wa Delhi, hutarajia kupata barabara zikiwa wazi namna hii.

Indian Prime Minister Manmohan Singh's official motorcade arrives to attend the Beating the Retreat ceremony in New Delhi on January 29, 2011.

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini kwa raia wa kawaida, barabara huwa hivi...

Travellers face traffic congestion on NH-24 as Kanwadias (Dak Kawad) carry holy water for Lord Shiva collected form the River Ganga, on August 1, 2016 in New Delhi, India. (P

Chanzo cha picha, Getty Images

... na hali huwa mbaya zaidi wakati wa mvua ya upepo wa msimu.

Magari yakwama kwenye foleni barabara kuu ya Delhi-Gurgaon Julai 28, 2016 mjini Gurgaon, India.

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alipofika Delhi kwa mashauriano na maafisa wa serikali Jumatatu jioni, hakuwa na bahati.

Mvua kubwa ilinyesha na 'kukosa kutambua cheo chake'.

Badala ya magari yake kupitia barabara zilizo wazi, msafara wake wa magari ulikwama kwenye foleni zaidi ya saa moja.

Lilikuwa jambo lisilo la kawaida kwa sababu maafisa wa usalama huondoa magari barabarani kutengeneza njia ya kutumiwa na wageni mashuhuri.

NewsX

Chanzo cha picha, NewsX

Watu kwenye mitandao ya kijamii walianza kufanyia mzaha masaibu hayo ya Bw Kerry. Baadhi, kama Karthik hapa alipendekeza Bw Kerry afanye wafanyavyo wenyeji mvua ikinyesha.

John Kerry

Chanzo cha picha, Karthik

Helikopta http://goo.gl/QLG66e

Chanzo cha picha, Rajesh Mahapatra

Maelezo ya picha, Bw Mahapatra alipendekeza serikali serikali inunue helikopta za kuwasafirisha wageni mashuhuri