Wageni 10 washikiliwa Uturuki wakihusishwa na mapinduzi

Uturuki imesema inawashikilia watu kumi wenye asili ya kigeni walioingia nchini humo kinyume na sheria, na kuhusika kwenye jaribio la kimapinduzi mwezi uliopita.

Raia hao wa kigeni hawajajulikana utaifa wao lakini serikali imesema mmoja wao alihukumiwa baada ya kuingia kinyemela akitokea nchini Syria.

Zaidi ya watu elfu kumi na nane wametiwa kizuizini wote wakihusishwa na kuhusika kwenye mapinduzi. Mhubiri mkuu Fethullah Gullen anatuhumiwa kuunga mkono mapinduzi hayo.