Kundi la Brics ni nini na malengo yake ni yapi?

A Brics signboard and cut-out of Nelson Mandela at the summit venue in Johannesburg in July 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, South Africans walk past an advertisement for a Brics summit which features an image of Nelson Mandela

Viongozi wa kundi la mataifa ya Brics - Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini - wamekutana tarehe 22 Agosti mjini Johannesburg, na suala kuu litakuwa ikiwa ni kukubali wanachama wapya.

Taifa mwenyeji wa mkutano huo, Afrika Kusini, limesema kuwa nchi 40 au zaidi sasa zinataka kujiunga na kundi hilo.

Kundi la Brics liliundwa vipi?

Mnamo 2001, mwanauchumi katika benki ya uwekezaji ya Goldman Sachs, Jim O'Neill, aliunda kifupi "Bric" kwa Brazil, Urusi, India na China.

Ni nchi kubwa, zenye kipato cha kati ambazo zilikuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi wakati huo. Alitabiri kuwa wanaweza kuwa nchi zinazoongoza kwa uchumi duniani kufikia 2050.

w

Mnamo 2006, nchi hizo nne ziliamua kujiunga pamoja kama kikundi cha Bric. Afrika Kusini ilijiunga mwaka 2010 na kuifanya kuitwa kundi la Brics.

Kundi la Brics lina umuhimu gani?

Kwa pamoja, nchi za Brics zina idadi ya watu bilioni 3.24 na mapato yao ya kitaifa yanafikia $26trn. Hiyo ni 26% ya uchumi wa dunia.

w

Hata hivyo, kwa mujibu wa Baraza la Atlantic, shirika la wataalam la Marekani, mataifa ya Brics yana asilimia 15 pekee ya haki za kupiga kura katika taasisi kuu ya kifedha ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Je, lengo la kundi la Brics ni nini?

Brics iliundwa kutafuta njia za kuleta mageuzi katika taasisi za fedha za kimataifa kama vile IMF na Benki ya Dunia, ili kuunda "sauti kubwa na uwakilishi" kwa mataifa yanayoibukia kiuchumi.

Mnamo mwaka wa 2014, mataifa ya Brics yalianzisha Benki Mpya ya Maendeleo (NBD), yenye fedha za $250bn, ili kukopesha mataifa yanayoibukia fedha kwa ajili ya maendeleo.

Nchi zisizo za Brics kama vile Misri na Falme za Kiarabu zimejiunga na NBD.

Je, nchi za Brics zitatengeneza sarafu ya pamoja?

Wanasiasa wakuu nchini Brazil na Urusi hivi majuzi wamependekeza kuunda sarafu ya Umoja wa Brics, ili kupinga utawala wa dola ya Marekani katika biashara ya kimataifa na fedha.

Hata hivyo, balozi wa Afrika Kusini katika Brics na Asia, Anil Sooklal, amesema haiko kwenye ajenda ya mkutano wa Johannesburg.

Jim O'Neill wa Goldman Sachs, ambaye kwanza alikuwa na wazo la nchi za "Bric", ameliambia gazeti la Financial Times la Uingereza kwamba wazo la sarafu ya pamoja ni "ujinga".

Brazilian President Luiz Inacio Lula da Silva inspects an honour guard with Chinese President Xi Jinping in Beijing in April 2023

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuwa mwanachama wa Brics huipa Brazil hadhi maalum kama mshirika wa kibiashara na China

Je, nchi za Brics zinafanana nini na ni nini kinachozigawanya?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kila mataifa ya Brics ni nchi kuu katika eneo husika, anasema Profesa Padraig Carmody, mwanajiografia wa maendeleo katika Chuo cha Trinity Dublin.

"Hata hivyo, China imekuwa taifa kubwa," anasema. "Kupitia Brics, inajifanya kuonekana kama sauti inayoongoza ya Global South, ikitoa wito wa mageuzi au kupinduliwa kwa utaratibu uliopo wa kimataifa."

Hata hivyo, India ni mpinzani wa China katika eneo la Asia-Pasifiki. Ina migogoro ya muda mrefu ya mpaka na China, na imekuwa ikifanya kazi na Marekani na wengine kuangalia upanuzi wa ushawishi wake katika kanda.

Mataifa ya Brics pia yamegawanyika kuhusu jinsi yanavyoyachukulia mataifa ya Magharibi.

"Urusi inaiona Brics kama sehemu ya mapambano yake dhidi ya nchi za Magharibi, na kuisaidia kushinda vikwazo wanavyoiwekea kwa kuivamia Ukraine," anasema Creon Butler, Mkurugenzi wa Mpango wa Uchumi wa Kimataifa na Fedha katika Taasisi ya Wataalamu yenye makao yake makuu London, Chatham House. .

 Aerial view of crude oil tanker 'VIEIRA' unloading oil at the 300,000 tonne crude oil terminal of Yantai Port on 19 October 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Urusi sasa inauza nje sehemu kubwa ya mafuta yake ghafi kwa washirika wa Brics India na China

Kufuatia vikwazo vya mataifa ya Magharibi juu ya uagizaji wa mafuta ya Urusi, India na China zimekuwa wateja wakubwa wa mafuta hayo.

Urusi pia ilifanya mazoezi ya pamoja ya wanamaji na China na Afrika Kusini mnamo Februari 2023.

Hata hivyo, wanachama wengine wa Brics hawataki iwe mkataba wa kupinga Magharibi.

"Afrika Kusini, Brazili na India hazitaki dunia iliyogawanyika," anasema Bw Butler. "Kuzipinga nchi za Magharibi itakuwa mbaya kwa usalama na ustawi wao."

Je, ni nchi gani zinazotaka kujiunga na Brics?

Balozi wa Afrika Kusini katika kundi la Brics na Asia, Anil Sooklal, hivi karibuni alisema kuwa nchi 22 zimeomba rasmi kujiunga na kundi hilo, na idadi hiyo hiyo imeonyesha nia ya kujiunga.

Ramani
At a meeting in China in 2019, Foreign Minister Wang Yi shakes hands with Iran's Foreign Minister Mohammad Javad Zarif

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Iran imeomba kujiunga na kundi la Brics

Nchi hizi ni pamoja na Iran, Argentina, Cuba, Kazakhstan, Ethiopia, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Venezuela.

"Kuna dhana kwamba uwiano wa mamlaka unaondoka kutoka Magharibi, na nchi nyingi zinazoendelea zinatazamia kupata mamlaka kama nchi za Brics," anasema Profesa Carmody.

"Lakini Brics ni kundi la kipekee," anasema. "Je, kukubali wanachama wapya kutapunguza ushawishi wake?"

"Nadhani yangu ni kwamba mataifa machache yataruhusiwa," anasema Bw Butler. "Lakini yatakuwa mataifa kama Argentina, badala ya mataifa magumu kama Iran."

Je, nini kitajadiliwa kwenye mkutano wa Brics?

Mkutano wa 2023 wa viongozi wa Brics unafanyika Johannesburg kuanzia tarehe 22-24 Agosti.

Kuamua sheria za nani anaweza kujiunga na kikundi inaweza kuwa mada kuu ya mjadala.

Masuala mengine katika ajenda ni pamoja na: kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi; kupanua biashara, fursa za uwekezaji na uvumbuzi katika nchi zinazoendelea; na mageuzi ya mifumo ya utawala wa kimataifa ili kuzipa nchi zinazoendelea maamuzi zaidi.

Afrika Kusini imewaalika viongozi wa mkutano huo kutoka zaidi ya nchi 60 barani Afrika, Amerika Kusini, Asia na Karibiani.

Walakini, Rais wa Urusi Vladimir Putin hatakwenda. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imetoa kibali cha kukamatwa kwake kwa uhalifu wa kivita, jambo ambalo amekanusha.

Afrika Kusini, kama mtia saini wa mahakama, italazimika kuitekeleza iwapo angefika katika eneo lao.

Rais Putin amesema atahudhuria mkutano huo kwa njia ya mtandao wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, atakuwepo ana kwa ana.