Je, Ukraine inataka uhakika gani wa usalama kutoka NATO na washirika wake?

Dhana ya mfumo wa uhakika wa usalama wa kimataifa kwa Ukraine iimewasilishwa huko Kyiv, mji mkuu wa nchi hiyo. Kwa walioandaa wanaona hautaisaidia Ukraine pekee katika kukabiliana na uvamizi unaoendelea wa warusi, lakini pia kuhakikisha usalama dhidi ya uvamizi mpya wa Urusi katika siku zijazo.

Licha ya ukweli kwamba wazo hili litajadiliwa na wanaohusia - ambapo Urusi si miongoni mwao - tayari imesababisha wasiwasi huko Moscow. Ikiwa mapendekezo yaliyofanyiwa kazi huko Kyiv yanaungwa mkono na washirika, hasa nchi za Magharibi, tutazungumza juu ya kasi ya kijeshi ya Ukraine na ushirikiano wake wa kina na NATO bila kuacha kuangazia hatua yake ya kujiunga na Umoja huo katika siku zijazo.

Hata hivyo, wataalam waliohojiwa na BBC walitathmini matarajio ya utekelezaji wa Mkataba wa Usalama wa Kyiv kwa utata. Pasi na shaka kwa upande mmoja, ni mkataba bora kuliko mkataba wa Budapest, ambao ulipaswa kutoa uhakika wa usalama wa Ukraine baada ya kuachana na silaha za nyuklia.

Kwa upande mwingine, huko Kyiv wamejiingiza katika uundaji wa muundo wa usalama, ambao hauna mfano katika ulimwengu wa kisasa, na sio ukweli kabisa kwamba utafanya kazi kama vile waundaji wake wanavyopendekeza.

Budapest - Istanbul - Kyiv

Mwanzoni mwa miaka ya 90, baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, Ukraine ikawa mmiliki namba mkubwa wa silaha za nyuklia ulimwenguni.

Kwa sababu tofauti, Kyiv alilazimika kuachana na mpanho huo. Kisha, kwa mara ya kwanza katika historia ya Ukraine, kulikuwa na mazungumzo ya kuipa nchi hiyo uhakika fulani ya usalama dhidi ya nchi zenye nguvu. Baadae vitaya sasa imeendelea kuthibitisha hilo.

Ilikuwa ni sababu ya kusainiwa kwa Mkataba wa Budapest mwaka 1994. Ndani yake, Marekani, Uingereza na Urusi ziliahidi kuheshimu uhuru na mipaka ya Ukraine, kujiepusha na matumizi ya nguvu na shinikizo la kiuchumi dhidi yake, na kutafuta hatua za haraka kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwa Ukraine inakabiliwa na hatari yoyote.

Kuingizwa kwa Crimea na kuanza kwa mzozo huko Donbas mnamo 2014 kulionyesha kuwa Mkataba wa Budapest ulizaliwa ukiwa mfu.

Siku moja kabla ya kuanza kwa vita, mnamo Februari 23, Volodymyr Zelensky alisema katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na viongozi wa Poland na Lithuania: "Sio siri kwamba Mkataba wa Budapest haufanyi kazi ... tunajitetea wenyewe kwa msaada kutoka kwa washirika wetu. Lakini ni watu wa Ukraine wanaokufa, Kwa hiyo, Ukraine inahitaji ukakika wa usalama, ulio wazi, thabiti, na sasa."

Ukakika mpya wa usalama

Kwanza kabisa, walioandaa mkataba huo wa uhakika wa usalama wanakubali, kwamba mfumo wa kipekee wa usalama anaoujenga unaweza kuchukuliwa kama ni wa mpito: mapema au baadaye Ukraine itajiunga na NATO na kujiunga pia na mfumo wa usalama wa pamoja wa Muungano huo unaojulikana - "mmoja kwa wote na wote kwa mmoja."

Waraka huo unasema ili Ukraine iweze kujilinda, inahitaji rasilimali ili kudumisha vikosi vyake vingi vya kijeshi, uwekezaji katika uwanja wake wa kijeshi na viwanda, uhamishaji mkubwa wa silaha na mazoezi makali kwa jeshi lake chini ya usimamizi wa EU na NATO.

Kwa hiyo, mapendekezo yanaeleza zaidi, kundi la nchi wadhamini wanapaswa kujitolea:

  • Kutoa msaada wa kifedha kwa Ukraine ili kusaidia bajeti yake ya ulinzi
  • Kutenga fedha ya maendeleo kijeshi na viwanda ya Ukraine.
  • Kuhamisha teknolojia kwa ajili ya uzalishaji wa silaha kwa Kyiv na kuiuzia silaha Ukraine
  • Kufanya mafunzo ya mara kwa mara ya jeshi la Ukraine
  • Kutekeleza mpango wa kukabiliana na vitisho vya mtandao mara kwa mara
  • Kupeana taarifa za kiintelijensia

Mkataba huo unarejelea vikosi vya ulinzi vya eneo, "ambavyo vitajumuisha raia wote walio na umri wa zaidi ya miaka 18." "Kile ambacho Putin hakutaka." NATO inaichukulia Urusi kuwa tishio kubwa zaidi.

Katika mapendekezo yaliyotolewa huko Kyiv, orodha ya wadhamini wametajwa kama ifuatavyo: "Nchi kama Marekani, Uingereza, Kanada, Poland, Italia, Ujerumani, Ufaransa, Australia, Uturuki, nchi za Ulaya Kaskazini na Baltic. Mataifa ya Ulaya ya Kati na Mashariki yanaweza kujiunga na makubaliano hayo - lakini orodha si kamili", Anders Fogh Rasmussen aliambia BBC.

"Dunia itaungua na itayeyuka kama saruji "

Wakati huo huo, Moscow ilijibu kuhusu uchapishaji wa rasimu ya mfumo wa uhakika wa usalama kwa Ukraine. Dmitry Medvedev, naibu katibu wa Baraza la Usalama la Urusi, aliuta mkataba huu kama "utangulizi wa vita vya tatu vya dunia."

Msemaji wa Rais Vladimir Putin, Dmitry Peskov, alisema kwamba "hati iliyoandaliwa na mamlaka ya Kyiv" inafanya "kutekeleza operesheni maalum ya kijeshi" kuwa muhimu zaidi.

Nini kinafuata?

Kama Anders Fogh Rasmussen alivyoambia BBC, wakati wa kuandaa mapendekezo ya mkataba huo, kwa makusudi hawakushauriana na serikali za nchi ambazo, kulingana na wazo lao, zinaweza kuwa wadhamini wa usalama huo wa Ukraine.