Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nchi ya Kiislamu inayotaka kuingia kwenye orodha ya nchi zenye nguvu zaidi kiuchumi duniani
Wanandoa wengi ambao ni vijana wanataka kustaafu wakati ni sawa, lakini Musmulyadi, mwenye umri wa miaka 55, na mke wake Nurmis, mwenye umri wa miaka 50, wanataka kuvunja mila hii.
Wamesafiri zaidi ya kilomita elfu moja kuutoroka mji mkuu mpya wa Indonesia, unaoendelea kukua kwa kasi.
"Kuna kazi nyingi ya kufanywa hapa, kwa sababu mji unajengwa sasa," alisema Musmulyadi, alipokuwa akiiambia BBC.
Sasa anajenga katika eneo la Nusantra, kama eneo la Borneo linavyoitwa ambalo limejaa watoto wa Java.
Nurmis anachanganya saruji huku Musmulyadi akiweka vigae.
Lengo lao ni lengo la Indonesia - Musmulyadi anatarajia kukamata ardhi katika kazi yake na kuwa mkandarasi mkuu katika mradi huu mkubwa.
Tangu Rais wa nchi hiyo, Joko Widodo, anayefahamika kwa jina la Jokowi, atangaze ujenzi wa Nusantra miaka miwili iliyopita, mambo ya biashara yanaendelea kupamba moto.
Mradi ambao serikali inaufanya katika jiji hilo ambapo watu milioni mbili wanatarajiwa kuishi ndani yake ifikapo mwaka wa 2029.
Lakini umbali wa kilomita moja, Pandi mwenye umri wa miaka 51 na mkewe Symsiah wana wasiwasi kuhusu kufukuzwa kutoka mahali pao.
Wanatoka katika moja ya makabila 20,000 katika eneo hilo, na hawana uthibitisho wa umiliki wa ardhi, ambapo familia yake imekuwa ikiishi kwa miaka.
Pandi aliamka asubuhi moja na kuona kwamba kijiji chao kilikuwa kimevamiwa, bila kupewa muda wowote wa kuondoka.
Serikali ilitaka kubomoa kijiji chao ili kuzuia mafuriko, lakini Februari Pandi aliizuia kutokana na kesi aliyopeleka mahakamani.
"Ninapigania hili kwa ajili ya watoto wetu wajao na wajukuu," aliambia BBC.
"Nikishindwa kufanya lolote, watoto na wajukuu zangu hawatakuwa na thamani serikalini. Ndio maana tunapambana dhidi ya dhuluma."
Hapa ni pahali pa kuishi kwa watu wa kijiji chetu kitambo, maana baadhi ya vijiji vilivyopo mbele yetu vimejengwa, baada ya serikali kuwalipa fidia, lakini kwetu hakuna.
Hadithi za Pandi na Mulyadi zinaonyesha jinsi kazi ya Rais Widodo ilivyo na pande mbili, nzuri na mbaya, kushinikiza wengine, na kuunda kazi kwa wengine.
Kujiunga na orodha ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ya nchi tano zenye nguvu zaidi kiuchumi Indonesia ilikuwa nchi ya 10 nafuu zaidi duniani ilipoingia kwenye orodha kwa mara ya kwanza mwaka 2014.
Miaka 10 baadaye, nafasi ya Indonesia imesogea hadi nafasi ya saba, nyuma ya China, Amerika, India, Japan, Ujerumani na Urusi.
Ifikapo mwaka 2027, nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani, inatazamia kuipita Urusi kwa nguvu za kiuchumi.
Nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia ilifanya uchaguzi wa rais mnamo Februari 14, ambapo takwimu zisizo za kiserikali zilionyesha kuwa Waziri wa Ulinzi Prabowo Subianto alikaribia kushinda uchaguzi katika duru ya kwanza.
Aliahidi kuendelea kukuza uchumi wa nchi kama anavyofanya rais wa sasa, na mtoto wa Rais Widodo, Gibran Rakabuming Raka, ni mmoja wa wagombea.
Nchi hii ina matamanio makubwa ya kuwa miongoni mwa nchi tano bora kiuchumi ifikapo 2045, wakati itaadhimisha miaka 100 ya uhuru.
Ili kufikia lengo hili, uchumi wa nchi unapaswa kukua kwa asilimia 6 hadi 7 kila mwaka.
Njia hii ilichukuliwa kwa sababu sasa inaongezeka kwa asilimia 5.
'Mlima wa Nickel'
Indonesia ni maarufu kwa kisiwa chake cha likizo cha Bali, lakini pia ina kiasi kikubwa cha chuma, ambacho hutumiwa kutengeneza betri za gari.
Rais Widodo alipotangaza kupiga marufuku uchimbaji madini ya nikeli mwaka wa 2019, Umoja wa Ulaya uliipeleka Indonesia kwenye Shirika la Biashara Duniani.
Rais alisema anataka kuboresha uzalishaji wa madini nchini Indonesia.
Hati iliyotolewa na kikundi huru cha utafiti, Kituo cha Utafiti wa Maendeleo ya Uchumi, ilisema kuwa mfumo mpya ambao alikuja nao kwenye Nickel umeunda nafasi za kazi na ukuaji wa uchumi.
Indonesia inategemea sana wawekezaji kutoka China kujenga mradi wa Neckel.
Rais Widodo amekosolewa kwa namna alivyoipa China fursa ya kuwekeza, huku akisahau kinachoweza kutokea kuiangamiza nchi hiyo na matatizo ya kiafya yanayoweza kutokea na matatizo ya mazingira ambayo mradi huo ungesababisha.
Matumaini ya kujenga
Wasiwasi ulizuka wakati Rais Widodo alipotia saini sheria mpya ya kuhamisha mji mkuu hadi mahali pengine mwaka wa 2022, wakati nchi hiyo ilikuwa ikipambana na Corona.
Nchi nyingi kama vile China zimeonyesha nia ya kuwekeza katika mji huo mpya, lakini hakuna kitu halisi ambacho kimejadiliwa hadi sasa.
Rais amejaribu njia nyingi ili kutimiza ndoto ya nchi hiyo ikiwemo sheria ya kuwasaidia wawekezaji jambo ambalo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema ni ukiukaji wa haki za binadamu.
Kwa mujibu wa habari, atakabidhi madaraka Oktoba, na kazi hii kubwa ya Nusantara itaonekana kuwa ni ushujaa wake
Imetafsiriwa na Jaison Nyakundi