Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 08.01.2024
Mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe, 25, amekubali dili la kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa kandarasi yake. (Foot Mercato - Kwa Kifaransa)
Madrid wamempa Mbappe, ambaye mkataba wake na PSG unamalizika msimu huu wa joto, kiasi kidogo cha pesa kuliko walivyofanya katika mazungumzo yao mwaka 2022. (Athletic - usajili unahitajika)
Hata hivyo , Mbappe bado anaweza kuhamia Ligi ya Premia. (Times - usajili unahitajika)
Juventus wamejiondoa kwenye mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips kwa sababu ya ada ya mkopo na kiasi cha mshahara wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Fabrizio Romano)
Hatua hiyo ya Juve inaweza kuongeza nafasi ya Newcastle kumsajili kiungo huyo. (Mail)
Liverpool wanaweza kupata kiasi kikubwa cha fedha kiwa kiungo wa kati wa Uingereza Jordan Henderson, 33, atauzwa na Al-Ettifaq ya Saudi Arabia (Mirror)
Everton wameweka ada ya £60m kwa Amadou Onana huku Arsenal wakilenga kumnunua kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji, 22 (Football Insider)
Chelsea , Manchester United na AC Milan wote wanamtazama mlinzi wa Nice na Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24, lakini klabu hiyo ya Ufaransa inatumai kuendelea kumshikilia katika dirisha la uhamisho la Januari. (RMC Sport - kwa Kifaransa)
Barcelona wameripotiwa kupewa nafasi ya kumsajili kiungo wa zamani wa Manchester United na Uingereza Jesse Lingard. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ni mchezaji huru tangu alipoondoka Nottingham Forest mwishoni mwa msimu uliopita. (Sport - kwa Kihispania)
Mshambulizi wa kimataifa wa Uingereza Ivan Toney, 27, anasema "hajakamilisha biashara" anapojitayarisha kurejea Brentford baada ya kutumikia adhabu ya kusimamishwa kwa miezi minane kwa kukiuka sheria za kamari. (Mirror)
Juventus wako tayari kufungua mazungumzo ya kuongeza mkataba na kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 25. (Goal)
West Ham wataangazia uwezekano wa kumnunua mlinzi wa Wolves Muingereza Max Kilman, 26, ikiwa watachangisha fedha kwa kumuuza mlinzi wa Morocco Nayef Aguerd, 27, mwezi huu(Guardian)
Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff huenda akaondoka katika klabu hiyo ikiwa ofa sahihi itapatikana kwa Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 26. (Sun)
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah