Afcon 2023: Je, Ivory Coast, Nigeria, Misri, Ghana na Senegal zina nafasi gani katika Kundi A, B na C?

Chanzo cha picha, Getty Images
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 inaanza nchini Ivory Coast katikati ya Januari baada ya kuahirishwa ili kupisha msimu wa mvua Afrika Magharibi.
Huku Senegal ikitazamia kutetea ubingwa wao, muundo wa timu 24 unamaanisha kwamba timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu hadi hatua ya mtoano, huku timu nne bora zilizo katika nafasi ya tatu zikiungana nao.
Kulikuwa na mshtuko katika Kombe la Mataifa lililopita nchini Cameroon, huku Comoro na Gambia, mabingwa mara nne Ghana wakirejea nyumbani mapema, lakini tunaweza kutarajia nini kutokana na toleo la 34 la michuano hiyo ya bara?
BBC Sport Africa imezungumza na wachezaji, magwiji wa soka barani Afrika na waandishi wa habari ili kuangazia kundi A, B na C.
Kundi A - Ivory Coast, Nigeria, Guinea ya Ikweta na Guinea-Bissau
Wenyeji walipangwa na washindi mara tatu Nigeria na Guinea ya Ikweta, ambao walijiondoa mara kadhaa na kutinga robo fainali mara ya mwisho.
Guinea-Bissau, ambayo inalenga kusonga mbele kutoka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza, inakamilisha safu ambayo mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba anatarajia kuwa "ngumu sana".
"Hakuna kitu kama droo rahisi kwa sababu timu zote zinastahili kuwa hapa na zitapambana," Drogba, ambaye aliifungia Elephants mabao 65, alisema.
"Nigeria, pamoja na Victor Osimhen na wachezaji wote walio nao, ni timu kubwa. Hatupaswi kusahau timu nyingine mbili kwa sababu kuna vitu vya kustaajabisha kila wakati.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Nadhani mtaji wetu mkuu utakuwa kuzingatia mchezo wetu, timu yetu, nguvu zetu na kujaribu kusonga mbele. Ni juu yetu kufanya vizuri zaidi, kuwa nyuma ya timu yetu na kuhakikisha kombe linabaki nyumbani."
Nigeria ilikabiliwa na ukosoaji kutoka kwa mashabiki baada ya kutoka sare katika mechi mbili za kwanza za kufuzu kwa Kombe la Dunia la Fifa 2026 dhidi ya Lesotho na Zimbabwe mnamo Novemba, lakini kiungo wa Super Eagles Frank Onyeka anasema ni muhimu mashabiki kuwaunga mkono.
"Najua itawasumbua lakini bado tunahitaji msaada wao," kijana huyo wa miaka 25 alisema.
"Tunajua nini kinahitajika ili kushinda Afcon. Sare tulizopata katika michezo miwili iliyopita ni jambo ambalo tunahitaji kujifunza."
Wenyeji hao wa Afrika Magharibi walitoka katika hatua ya 16 bora nchini Cameroon na Onyeka anatarajia kibarua kigumu katika kundi lao lenye makao yake Abidjan.
"Timu za Afrika si rahisi kucheza dhidi yake," aliongeza. "Ni jambo ambalo tunahitaji kujitayarisha kiakili na kimwili."
Ratiba ya Kundi A
Jumamosi, Januari 13: Ivory Coast v Guinea-Bissau
Jumapili, Januari 14: Nigeria v Guinea ya Ikweta
Alhamisi, 18 Januari: Ivory Coast v Nigeria, Guinea ya Ikweta v Guinea-Bissau
Jumatatu, 22 Januari: Guinea ya Ikweta v Ivory Coast, Guinea-Bissau v Nigeria
Kundi B - Misri, Ghana, Cape Verde and Msumbiji

Chanzo cha picha, reuters
Misri wanatarajia kusafiri mbali Afrika Magharibi baada ya kupoteza fainali mbili kati ya tatu zilizopita za Afcon, dhidi ya Cameroon (2017) na Senegal (2021), baada ya "uchezaji bora wa kiufundi" kulingana na mwandishi wa habari wa Misri Inas Mazhar.
"Msumbiji inapaswa kutoa mwanzo wenye muendelezo kutokana na tofauti ya uzoefu na historia kati ya timu hizo mbili, lakini mchezo wa pili dhidi ya Ghana utakuwa mgumu na muhimu zaidi, ambapo Misri itapigana kujiweka kileleni," aliongeza.
"Pamoja na Cape Verde kufuata, nafasi ya Mafarao kuongoza kundi ni kubwa lakini kama watafuzu kwa robo fainali, Waafrika Kaskazini watamenyana na timu zenye nguvu zaidi.
"Kocha mkuu Rui Vitoria hajakabiliwa na mtihani kama huu tangu ashike wadhifa huo Julai 2022, ambayo inaweza kuwa changamoto kubwa zaidi kwa Misri.
"Mreno huyo atakabiliwa na uchunguzi wa mashabiki na wachambuzi wa soka wa Misri, ambao hawatakubali chochote zaidi ya kucheza fainali."
Matarajio makubwa pia ni suala la Ghana, huku mtangazaji wa BBC Sport na mwanahabari George Addo Jr akisema mashabiki "wana wasiwasi" na aina ya Black Stars, ambayo haijatinga hatua ya nane bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika tangu 2017.
"Ghana ilitolewa katika hatua ya 16 bora mwaka wa 2019 na haikushinda na ilishindwa kusonga mbele kutoka kwa hatua ya makundi nchini Cameroon," aliongeza.
"Changamoto ambazo timu ilikabiliana nazo zilionekana katika kufuzu. Upande huo haukuwa na muunganiko, timu ya ufundi ilionekana kutoridhika na kutojali kwa mashabiki kulionekana baada ya kufanya vibaya mara kwa mara.
"Black Stars wametatizika katika kipindi cha kwanza cha michezo yote iliyosimamiwa na Chris Hughton hadi sasa na bao moja tu kati ya tisa walilofunga chini yake likipatikana katika dakika 45 za kwanza."
Baada ya kuhitaji bao la ushindi dakika za mwisho ili kuishinda Madagascar katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia na kisha kushindwa huko Comoro, Addo Jr anadhani "hakuna hakikisho" kwa Ghana.
"Mechi dhidi ya Cape Verde na Msumbiji zimekuwa za wasiwasi kutokana na uchezaji dhidi ya wachezaji wadogo hivi karibuni," alisema.
"Kufuzu kwa robo fainali kutakuwa na mafanikio makubwa. Ingawa hilo linaweza kuonekana kufikiwa, Hughton na timu yake lazima watafute wachezaji 11 wa mwanzo XI wa kuaminika.
"Zaidi ya hayo, Black Stars itahitaji kuweka wachezaji muhimu katika hali ya utimamu ili kupata nafasi."
Ratiba ya kundi B
Jumapili, 14 Januari : Misri v Msumbiji, Ghana v Cape Verde
Alhamisi, 18 Januari: Misri v Ghana
Ijumaa, 19 Januari: Cape Verde v Msumbiji
Jumatatu, 22 Januari: Msumbiji v Ghana, Cape Verde v Misri
Kundi C - Senegal, Cameroon, Guinea na Gambia

Chanzo cha picha, Getty Images
Miamba, Cameroon wana mataji matano ya Kombe la Mataifa ya Afrika lakini walilazimika kushika nafasi ya tatu kwenye ardhi ya nyumbani mara ya mwisho.
"Tunawatarajia kuleta kombe nyumbani, hasa kwa sababu tulishinda Afcon yetu ya kwanza mjini Abidjan mnamo 1984," mchambuzi wa soka wa Cameroon Lawrence Nkede alisema.
Bado michuano ya fainali za 2021 yalizua maoni tofauti. Huku kukiwa na sifa ya uimara wa timu hiyo, hali ya kukata tamaa ilitanda baada ya kufungwa na Misri katika nusu fainali kwa mikwaju ya penalti.
Sasa waangalizi wana wasiwasi kuhusu kocha Rigobert Song kukosa kikosi cha kwanza kilichotulia.
"Katika michezo kumi iliyopita tumekuwa na safu kumi tofauti. Ni vigumu sana kuisoma timu na uwezo wake halisi," Nkede aliongeza.
Huku mlinda lango Andre Onana akistahimili kushuka kwa kiwango katika klabu ya Manchester United na mashaka juu ya utimamu wa mshambuliaji Bryan Mbeumo, huenda Simba tayari wamejeruhiwa kabla ya mechi yao ya kwanza dhidi ya Guinea.
Syli Nationale wametinga hatua ya mtoano katika mechi tatu zilizopita huku Gambia wakirejea baada ya kutinga robo fainali kwa kushtukiza katika mechi yao ya kwanza ya Afcon.
"Scorpions itabidi wawe katika ubora wao ili kusonga mbele kufuatia matokeo duni na kushindwa mara mbili katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia," mwanahabari Momoudou Bah alisema.
"Kikosi cha kocha Tom Saintfiet kitasukumwa kuchuana na Senegal katika mchezo wa derby katika mechi ya ufunguzi, kwani itakuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 15 nchi hizo mbili kumenyana katika hatua ya juu."
Soka ya Gambia inaendelea, huku nchi hiyo ikishiriki Kombe la Dunia la Vijana chini ya miaka 20 mwaka huu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16, lakini Saintfiet amekabiliwa na ukosoaji kuhusu falsafa yake ya uchezaji.
"Lakini amelazimika kukabiliana na msukosuko kutoka kwa mashabiki wanaotarajia ambao wanataka mbinu ya kupanuka zaidi. Saintfiet pia amekumbana na changamoto katika maandalizi huku baadhi ya wachezaji muhimu wakihangaika mbele ya lango."
Ratiba ya kundi C
Jumatatu, 15 Januari: Senegal v Gambia, Cameroon v Guinea
Ijumaa, 19 Januari: Senegal v Cameroon, Guinea v The Gambia
Jumanne , 23 Januari: Guinea v Senegal, The Gambia v Cameroon
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga












